Watanzania wana simulizi za kusisimua kuhusu asili yao. Hapo zamani za kale, kutokana na uso wa ardhi kutokuwa mgumu, ardhi ilipasuka na kusababisha Bonde la Ufa ambalo linatanda kuanzia kusini mwa Yemen kupitia nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania, hadi Ziwa Nyasa na kugawanyika magharibi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Moja ya sehemu mashuhuri sana katika Bonde hilo ikatokea ndiyo chimbuko la binadamu. Binadamu wa awali anafanana na nyani na kwamba fuvu lake na nyayo ziligunduliwa na familia ya Leakeys hapo mwaka 1959 na 1979. Ushahidi huu ambao ni matokeo ya uvumbuzi wa elimukale kuhusu binadamu wa kwanza ulipatikana katika Bonde la Olduvai na Laetoli. Maeneo hayo yalikuwa baadhi ya makazi ya ukoo safu wa kisasa (homo habilis na homo sapiens), wazee wa kitanzania ambao waliweza kufikiri na kutengeneza vifaa vinavyotokana na mawe. Mabaki muhimu ya vifaa na mifupa vilivyoachwa na aina ya binadamu, vinakadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni moja na sabini na tano elfu. Aidha, ushahidi kamahuo umechimbuliwa kwenye maeneo ya kihistoria huko Isimila katika Nyanda za Juu za Kusini ambako vifaa vya kale, vijulikanavyo kama shoka vinaweza kuonekana leo. Michoro kwenye mapango ya Kondoa-Irangi iliyochorwa na babu zetu hao na dalili za shughuli za uhunzi na umwagiliaji maji mashamba ni ushahidi mwingine wa kuwepo kwa dalili za mtu wa kwanza katika Tanzania kwa wakati wa kale. Ni vyema kusadiki na kukubali kutoka hapo ni kwamba baadhi ya wazao walitawanyika duniani kote na baadaye kurejea Tanzania kujiunga na dada na kaka zao waliobaki hapa nchini.
Utamaduni, mila na desturi
Hali
ya mvuto wa mfumo ya jamii wa Tanzania ni kivutio kikubwa kwa
masuala ya utamaduni, uchumi na utalii.
Hadithi za watu wa kale, ngoma za asilia na aina ya ngoma
zinatofautiana kati ya kabila na kabila.
Wanapocheza, Wamakonde kuchezesha viuno vyao kwenda
sambamba na ngoma ya “sindimba”, Wazaramo humezwa na
maandamano ya “mdundiko”.
Wamaasai huruka kwa mpangilio maalum huko wakitoa
sauti nzito ambazo zinaweza kumwogofya simba dume!
Matumizi ya nyoka hai na kucheza na nyoka wakubwa kama
chatu kunakofanywa na Wasukuma wakati wanacheza ngoma ya
“Bugobogobo” hakuwezi kusahaulika kwa mgeni.
Kila kabila kati ya makabila
120 ya Tanzania ina ngoma yake na staili zake za uchezaji ambazo
zinapumbaza kwa kukazia macho zinafurahisha na kuvutia kijinsia.
Wamasai Ni Watu wa Pekee Wanaovutia hapa kwetu Tanzania.


No comments:
Post a Comment